Mungu asimama katika kusanyiko la Mungu; Katikati ya miungu
anahukumu….Mimi nimesema, ndinyi miungu, na wana wa Aliye juu, nyote
pia. Lakini mtakufa kama wanadamu, mtaanguka kama mmoja wa wakuu.
PDF
Ni wajinga tu hufa; hili lawezakuwa ni jambo nzito kidogo kwa wengi
kwa sababu, la kwanza, linawezasikika kama kiburi na majivuno
mwanadamu anaposikia likisemwa lile, ambaye, pamoja na ulimwengu
aliomo yeye mwanadamu, unatukuza sana kifo na hata ule ulimwengu
hufanya maagano na kifo. Ndio, kwa njia moja au nyingine, wanadamu
wamekitukuza kifo, kukiinamia, na hata bila kujua wakasema,
“ewe kifo, nani kama wewe!”
Kabla yako kukasirika na kunipuuzilia mbali, utazame ule mstari tena;
“Ni wajinga tu hufa” na kile Yesu alisema alipowaambia
wayahudi wa kale, “walio wafu na wazike wafu wao”.
Hili lilikuwa ni jibu lake kwa mtu ambaye kwa unyonge na upole
alimwomba akaweze kumzika babake, halafu aje amfuate Yesu.
Kama wayaelewa waliyoyafanya wayahudi walipokuwa wanawazika wafu
wao, pamoja na sheria zilizoambatana na hayo za urithi, utaelewa ni
kwa nini huyo kijana mdogo alikwazika. Inamaanisha kuwa wao, na
vizazi vilivyokuwa mbele yao, Musa akiwemo, walikuwa ni wapumbavu,
wasiokuwa na maarifa, ambao walifungwa na tamaduni za kuwazika
waliokufa. Huyu kijana myahudi ambaye kwa muda aliuona mwanga wa
Nuru yake Yesu, na akatafuta kuyaambatonisha maisha yake na hiyo
Nuru, kwa ghafula anashtuliwa na usemi wake Yesu, na anarudi kwenye
kiza na asihesabiwe kati ya wafuasi waliomfuata Yesu, na basi
kuipoteza nafasi yake kwenye Mkono wa Kuume wa Utukufu.
Yesu, kama mwingine yeyote aujuae Ukweli na kutembea kwenye kwenye
Nuru hatakuwa na lolote liambatanalo na ulimwengu uegemeao kifo na
kuzimu.
Yesu hangekubali kuambatanishwa na hekaya na hadithi za kuomboleza
zitokazo kenye mavumbi ya makaburi, ila Yeye angeimba pamoja na
mbele ya ndugu zake katika nchi ya walio hai, wakiunena Upendo wa
Baba Yake aliyembariki na Baraka zote rohoni na akampa vitu vyote
kwa furaha yake. Alifunuliwa ili akafichue vilivyofichika katika
hali za kishetani na akavimalize kupitiamoto wa miguu Yake iletayo
Injili, kuwafungua ndugu zake kutoka kwa nira ili kuingia kwa uhuru
mkuu wa (M)wana wa Mungu.
Kwa ajili hii sauti kuu itokayo mbinguni, ikiambatana na ngurumo na
radi kwa walio kwenye nchi yasema, "Agano letu na kifo
litavunjwa na makubaliano yako na kifo hayatasimama tena".
Ni sauti hiyo hiyo ingurumayoiliyonena kupitia Yesu katika siku zake
za mwili na inayoongea wakati na majira haya kupitia malaika
(mitume) wake Mungu ambao wameambatana na kweli.
Kwa kweli, kubarikiwa ni wale ambao hawatakwazwa na Nuru hata
inapozima na kudunisha tamaduni na taratibu za mababu zilizokwezwa
na mipangilio ya wanadamu wa ulimwengu huu wa nje tuishio kati
mwake; nah ii Nuru yafanya vile kwa kumfunua Yeye Yule, Pweke
Aliyekatikati ya mambo yote.
Heri mtu Yule ambaye hana mashaka nami - Luka 7:23
Kumbuka kuwa, kumjua Huyu Ambaye Yohana amwashiria anaposema ‘lazima
akwezwe name nidunishwe’, ni lazima nishushwe mimi mwenyewe katika
utu wangu, na jumla ya imani zilizoko ndani ya utu ule ziwe bure.
Dunia lazima ijae na maarifa Yake Huyu kama vile maji huijaza
bahari, kwa sababu kando Yake hapana mwingine; hii ndio Siku ya Yeye
Aliye, wakati ambao kila vuli litatoweka na kutokomea na Yeye Aliye
kudhihirika. Tunaposimama kwenye Nuru, inadhihirika kwamba mambo
yote yaliyo nje yake ile Nuru ni vivuli tu na mafumbo. Ukiliona,
kuligusa, kuliita, kulionja, ujue kwamba hilo ni vuli na ni fumbo na
linamwashiria Yule Aliye sirini. Mwanadamu awezakuwa mjinga, abebaye
mizigo isiyostahili, mchovu na mwenye uchungu kwa njia zote zile
anapovikimbiza vivuli kila siku ya maisha yake. Katika Nuru, kila
kitu ambacho wanadamu hukishikilia kama cha dhamana katika ulimwengu
huu tuliomo, kwa ghafula hufanyika vinyago vichukizavyo na sanamu,
kwa sababu havijakitwa katika kweli.
…kwa maana kile kinachoonekana kuwa kitukufu mbele ya watu, Mungu
anakiona kuwa takataka - Luka 16:15.
Na kama tujuavyo, mara kwa mara, Yesu alikumbwa na pingamizi
kutokana na watawala na wafalme wa ulimwengu huu ambao
hawangestahimili mafunzo na mafundisho yake yaliyofunza kuwa kuna
Mungu tu, na Yeye Yesu ni mmoja na Mungu. Kwa nini hili liwakwaze
watu? Hili fundisho takasika linalomfunua Mungu kama yote ndani ya
yote ni kama Jiwe litupwalo, lililokatwa kutoka Milele ila sio kwa
mkono wa mwanadamu, na kuharibu na kutawanya uvumbini kila msingi wa
imani za wanadamu walizojikweza kwazo.
Katikati ya mojawapo wa nyakati zile za kupingwa kwake, Yesu, kwa
upole aliwakumbusha watesi wake kwamba yale maandiko
waliyoyashikilia kama jiwe-msingi na kina cha imani yao, yakiri
peupe kuwa wao wenyewe ni miungu, na wana wake Mungu Aliye Juu
zaidi. Yesu alikuwa akisema kwa udhahiri kuwa, "Ndugu zangu,
mmesahau kuwa sisi ni hali moja, Baba Mmoja, Uhai Mmoja, Utukufu
Mmoja; mmesahau kuwa pale mwanzo tulishangilia kwa furaha pamoja
katikati ya wana wake Mungu, na vile tuliimba kwa sauti zenye utamu
kati ya nyota za asubuhi".
Badala ya kuwatuliza, kuwakomboa na kuwaponya, hiyo miale ya Nuru ya
ufunuo halisi itiririkayo kutoka kwenye vilindi vyake Baba ilipepeta
miale ya moto wa kuwauguza na hasira hata walipotafuta kumsulubu
Kristo. Lile neno lililokuwa kama umande kwa mche mchanga, lilikuwa
liwaletee ukumbusho na kuwainua hadi hatima ya utukufu wao, lakini
kwa ghafula likawa kikwazo kwao, na uvundo mkuu wa kifo ukafanyika.
Wakawacha rehema iliyokuwa iwaletee wokovu, na kwa kufanya lile,
wakamsulubu Yesu Aliyekuwa Uhai Wao, kwao. Hawangewezaelewa na
kuikumbatia ile Nuru inayong’aa kwenye lile shimo lililo kenye
fahamu zao zenye kutiwa kiza, na kufuatia lile, wakafa kwa sababu ya
kutoamini kwao kama wanadamu tu wa kawaida. Hiyo Nuru ilikuwa
iwakomboe kutokana na nira ya kifo na iwape nguvu tena na zaidi kuwa
wana.
Ana mwanga huo huangaza gizani, nalo giza halikuweza
kuushinda…Lakini wale wote waliompokea na kumwamini, hao aliwapa
uwezo wa kuwa watoto wa Mungu. - Yohana 1:12.
Mwanadamu awezaje kwa ujinga na upofu kuukataa wokovu mkuu namna hii
unaotangazwa leo kwa kila kiumbe kilichoko chini ya mbingu. Mtu
awezawanyoshea kidole cha lawama waliohifadhi torati ya Musa na
imani ya Kihebrania nyakati za Yesu ilhali wao washindwa kutafakari
kwa undani. Hii ni nia ya waandishi wa torati na mafarisayo
inayodhihirisha fikra za mwanadamu zilizokita mizizi na
kufunganishwa na mambo makuu ya kishetani, na ambayo
hayawezikuzielewa siri za Uzao Wake Mungu, ambazo zimefichika chini
ya vuli za mifano tofauti ya wanadamu na miigo ionekanayo na
isiyoonekana. Ndio nia ile ile iliyonyonge na isahauyo, inayoelekea
kwa ubatilifu wa mambo ya kijinsia ambayo hata Yesu mwenyewe
alipigana nayo aliposimama katika pengo na kuifunua ile siri ya
Uungu wetu. Ndio nia ile ile inayojidhihirisha kama shetani,
itafutayo kumvutia na kumjaribu Mwana kupitia utukufu wa ulimwengu
upitao umfanyao yeye kuiacha hali yake ya kwanza, na kuukimbilia
utukufu wa ulimwengu Alipofunga. Baadaye, Yesu alisema, "…kwa
maana roho i radhi lakini mwili ni dhaifu", kwa maneno
mengine, ni nyonge na dhaifu kusikia na kuelewa mambo makuu ya
Mungu.
Akiandika kupitia kuongozwa na Roho, mwandishi wa Zaburi 82
azungumzia kuhusu siri kuu, KUSANYIKO LA MWENYE NGUVU – MUNGU MWENYE
NGUVU. Mwandishi wa Zaburi hii fupi alifunguliwa macho kuona kitu
ambacho yeye mwenyewe hakukielewa; alikuwa akiliangalia Kusanyiko –
Kanisa – Kusanyiko kutoka Dunia yote – Kusenyiko la Miungu katika
Jina la Baba. Haijanakiliwa kuwa Kusanyiko litakuwa kwake Bwana; ni
hivyo kwa sababu hilo Kusanyiko lilitokana na, na Chanzo Chake ni
Yeye Bwana. Hawa ndio haswa walio Mungu…Mwili wake Mungu; wanao
ukamilifu wa hali yao umefichika ndani Mwake Mungu, maana kuwa wao
waishi kwa niaba ya, na kupitia Yeye. Hawa ndio wale Kusanyiko
linalojitokeza kama Wingu juu ya maji likikiri, “na kuwe…”,
“natu…” Ndilo Kusanyiko la Mungu anayejitokeza tena kama Mtu
wa Kibingu asemaye, "Mimi Ndiye Mwenye Mamlaka yote, niishiye
milele, na pweke aliye nazo fungua za kuzimu na za kifo”.
Kuhusu huu umati wa wana wa Mungu yesu asema, kifo hakina nguvu; kwa
maneno mengine, hawawezi kufa.
Yesu atukumbusha tena kuwa tulikuwa katika hilo kusanyiko la Mwenya
Nguvu na Milki Yote anaposema, "Ulikuwa Nami tangu mwanzo"
(Yohana 15:27). Kama hili laashiria chanzo cha kila
mwanadamu, basi kwa nini mwanadamu afa? Kwa nini waonekana kama
wamepungukiwa na hatima ya kilele cha Mungu? Zaburi 82 inatupa
jawabu lililo rahisi: "Hawajui, wala hawatafahamu; watembea katika
kiza: pale “…misingi yote ya nchi imetikisika".
Twawezahatimisha haya kwa misemo mitatu, ‘bila maarifa’, ‘bila
kuelewa’, ‘upofu rohoni’. Yadhihirisha upumbavu wa kiroho
uliowakamata wanadamu walio kwenye ulimwengu huu ambao wanaipoteza
milki yao ya kiungu. Katika kutoelewa kwao na kutiwa kiza,
wamefanyika tu watu wanaokufa na kwa hivyo wao wafa kama wanadamu.
Nalafu baada ya pale yasikika sauti ya mzika wafu ikisema,
“nyinyi ni mavumbi…..”
Watu wangu huangamia kwa kukosa maarifa: kwa sababu mmeyakataa
maarifa (Hosea 4:6)
Twaweza sasa kuelewa ya kuwa (m)wana wa Mungu Aliye Juu ni wa ile
hali isiyoharibika nay a milele kama Babaye wa Mbinguni, na kupitia
lile, kifo hakiwezimshikilia. Baba wa Nuru yote asema, “ndani
mwangu sina kifo, kwa hiyo siwezikitoa nisocho nacho, mbali mimi
hukifufua kilichokufa na kukisafirisha hadi Uzimani. Katika Ufalme
wangu uharibifu haujawahisikika; hakuna kidanganyacho katika Ufalme
wangu.” Kinachozaliwa na Mbegu isiyoharibifu pia ni
kisichoharibika na cha umilele na huzaa matunda yaambatanayo na ule
Uzima kulingana na mfano wake.
Mjinga ni nani, isipokuwa yeye aiachaye hali yake ya kwanza kwa
kutoyahifadhi maarifa ya Bwana wa uhai wake. Akikiri kuwa yeye ni
mwenye hekima katika njia za kilimwengu, yeye basi huiondokea kweli
na maarifa ya Hali yake halisi, Bwana asiyeonekana na asiye na
uharibifu, na kuibadili kwa kile kinachoharibika. Ni hali ile ile
katika habari ya wana wa Mungu nyakati zake Nuhu waliodanganywa na
ubatili wa mali (ambao ni ukawaida), wakaiacha hali yao ya utukufu
na kushuka ili kuungamanika na walio na mwili, na baadaye
wakafutiliwa kuingia vilindini vya njia za mauti. Wakijidhania kuwa
wenye hekima, wakafanyika ukamilifu wa ujinga wakijiharibu wenyewe
kwa kuuwacha utukufu wa maarifa ya Mungu Muumba wao na
kujiambatanisha na kilichoumbwa, na ndicho chanzo cha kufa kifo cha
wanaadamu. Yasikie maneno yake Roho: "itamfaidi nini mwanadamu
akijitwalia taifa na utukufu wa ulimwengu huu tu na kuipoteza nafsi
yake kwa nguvu za kaburi?"
Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na
kuyafanya chukizo. Hakuna atendaye mema. Toka mbinguni Bwana
aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye
Mungu. - Zaburi 14:1-2.
Yatafakari haya, hakuna hata mwanadamu mmoja chini ya mbingu
anawezajisitiri kutokana na ubatili huu wa kuyakataa maarifa Yake
Mungu. Kama wangeyahifadhi haya maarifa Yake Mungu hawangekuwa watu
wafungwao duniani. Badala yake wangekuwa wana wake Mungu walio na
kweli ya uzima wao ndani Yake katika mbingu. Makaazi yetu halisi ni
ni Ndani Yake, katika mbingu, ambazo ni Ufalme wake Mungu. Tunapojua
haya, kama Yesu tunawezasema bila tone lolote la shaka kuwa sisi si
wa ulimwengu huu tulio: Hata ingawa kwa muda tunawezapatikana ndani
yake, sisi sio wa ulimwengu huu. Kwa ajili ya hili pekee, mtumishi
wake Mungu anatangaza Habari Njema na ya Milele ya Upatanisho kwa
waishio ulimwenguni ambao wamepotoka na kuiondokea hali yao ya
mwanzo ndani Yake Mungu, akisema, “tubuni na mkamrejelee Bwana
wa Uzima wenu; mkapatanishwe Naye ili muokolewe”.
Kisha nikaona malaika mwingine, akiruka katikati ya mbingu, mwenye
injili ya milele, awahubiri wao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na
kabila na lugha na jamaa, akasema kwa sauti kuu, Mcheni Mungu, na
kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye
aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemichemi za maji. -
Ufunuo 14:6-7.
Tambua kwamba hii injili njema imeelekezwa kwa wale wanaoishi
ulimwenguni wala sio kwao wanaoishi katika mbingu ambamo
linapatikana Kanisa. Kupatikana, au kuishi ulimwenguni kwa hakika
yamaanisha kuwa wa kilimwengu, kijinsia na kuwa na nia batilifu ya
kiwanadamu, ambayo ndio maana yake kifo. Habari Njema ni kwamba
imeundwa kiasi kwamba inaleta uvuvio, nuru na upatanisho, ili wana
wake Mungu wakawezejitambua tena katika uridhi wao katika kusanyiko
la kibingu lake Mungu.
Wana wake Mungu, amkeni toka wafu na mkaamini tena katika lile Jina
Moja; kwa imani mkabatizike katika hio utambulisho huo wa Bwana wa
Utukufu. Mkaipokee Habari Njema ya Neema inayofunua huu ushirika
uliofichika ndani Mwake Mungu, ambao hata wewe ni mshirika. Usikie
ujumbe wake mtumishi na uishi.
Akinena kwa Jina la Baba, Yesu aliendelea kukiri, "awaye
yeyote asiyeamini kwamba Mimi Ndiye, atafa katika dhambi zake".
Linganisha maneno haya yake Yesu na hili: "mshahara wa dhambi
ni mauti". Kupitia yote haya, tunapata kuona kuwa Yesu
anatupa maana mpya ya dhambi, inayofutilia mbali kile ambacho
wanadamu waliita dhambi. Na ndicho hiki; Dhambi ni kukosa kwake
yeyote kujitambua katika ukweli na utambulisho wake halisi kama
mwanaye Mungu ambaye ndiye mmoja naye Baba. Ni kama kujiambatanisha
na hali nyingine ambayo ni ubinafsi wa kimwili. Kutoamini pekee ni
dhambi, na ndio maana anasema, “Amini na uokolewe”.
Uamini nini? Uamini kuwa Yeye Aliye, Ndiye Yuko ndani yako na Yeye
Ndiye ayaaye sayari yote. Ukawezaamini hili, unaweza basi kuingia
katika Upumzisho Wake kama vile Mungu Mwenyewe alivyopumzika, kwa
sababu jangwa la uharibifu, ambalo lalinganishwa nakutoamini
labadilishwa kuwa Shamba liotao mema – Edeni. Mtoe adanganyaye,
asemaye uongo na uamini tena.
Kutoamini huleta kifo, hali iendeleayo na kumwangusha asimamaye
kutoka kwa Chanzo chake, "BWANA MUNGU WAKO"; ni mwanguko usiokoma
unaoelekeza kwenye shimo la utupu ambamo kujua kilichochema na
kirembo, na chenye utukufu wa Uzima wa Mungu hupotea. Mwanadamu
asipojitambua kuwa mwana mpendwa wake Mungu, ampendezaye na
asiyehukumika mbele Zake, yeye ataadhirika na kuugua katika mateso
yaongezekayo ya mauti na kifo. Kushindwa kuyasikia maagizo na
maelekezo yanayosaidia kumtafuta Mtakatifu Aliye Ndani, ambaye
chanze Chake ni Umilele, humfanya huyu mwana kufa kama mwanadamu.
Akizidi kuishi katika ubatili huu wa kutokumbuka mahali pake katika
zile nyota za sayari zizungukazo, ataishi kutangatanga katika kiza
kisichoisha, mbali na mahali pake pafaapo katika vilele vitakatifu
Vyake Mungu, mahali pa nguvu zote.
Yatafakari haya, "…kwa sababu ya upendo usiopimika Wake Mungu
kwa ulimwengu, Amemtoa Mwanawe Pekee ili ulimwengu ule usiangamie”.
Ulimwengu ni ule ulioondokea ukweli wa ushirika wa umoja
wake Baba na Mwana na kwa hilo kufanyika kipofu kwa ile kweli kuwa
“MIMI NDIYE”; hii ndio maana ya kifo. Mwanadamu awezajepindua
au kuigeuza hii hali? Ni rahisi, kuipokea karama yake Mungu bure,
ambayo sio lingine ila kukubali kuwa yeye ni Mwana. Na kwa utiifu
kuifuata Sauti ya Yule Upako na kuzifungua ile mihuri iliyoifunga
fahamu yako; mkubalishe aliye Ndani ainuke na atokeze. Usimwache
adanganyaye adanganye tena, mfurushe autawalaye ulimwengu huu
apingaye kurejea kwako kwa mahali pako pafaapo katikati mwa Edeni.
Ukawe na furaha kila wakati kwa sababu Baba wa Nuru yote ametupa
nuru, itufanyayo wenye hekima machoni pake. Cha kustaajabisha ni
kuwa hiyo hiyo hekima tunayoipokea kutoka juu kila wakati itasikika
ni kama ujinga kwa walio nje kwa sababu imefichika kutoka kwao.
Walio na hekima machoni pa Mungu, hata ingawa wao huonekana wakiwa
wajinga na wapumbavu kwao walio nje, wao huivumbua njia ya utakatifu
kuurejelea Uzima, mahali ambapo kifo hakipo tena. Wao husimama
milele kwenye patakatifu wakiwa wajitambua tena katika Bwana. Ndani
Yake hamna kifo tena, wala tunda lake ambalo ni huzuni, uchungu na
kuomboleza; nao huu ndio Uzima wa Milele. Inuka na ufufuke kutoka
kwa wafu na ukatawale katika Uzima; furahia haya!
Ana hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya
utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya
watu hoa; wasifirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia
hiyo. Hapo hawatakuwa na samba, wala mnyama mkali hatapanda juu yake;
hawataonekana hapo; bali waliokombolewa watakwenda katika njia hiyo.
Na hao waliokombolewa na bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba;
na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko
na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia.-
Isaya 35:8-10
Wenu,
Trevor Eghagha, wa Huduma ya Sunray.
www.sunrayministry.org